Wanandoa waliozaliwa siku moja,wamedumu miaka 75 na wamefariki mwezi mmoja uliotenganishwa na siku!

Mapenzi yanakuwa mazuri na matamu pale kunapokuwa na uaminifu utakaofanya mdumu na kuweka historia nzuri hata kuwa mfano wa kuigwa!

Wanandoa Helen na Les Brown (94) kutoka California wameweka historia nzuri ya mapenzi yao maana wamezaliwa siku moja, wameoana na kudumu kwenye ndoa kwa miaka 75 na wote wamefariki mwezi uliopita yaani  Helen kafariki July 16 akafata Les July 17!



Kama wapenzi wengine walivyo,watoto wao wana sema Browns walikuwa na matatizo yao ila waliweza kuvuka vikwazo na kufanikiwa kudumu mpaka kifo kilipowatenganisha.Helen alifariki kutokana na kansa ya tumbo wakati Les akisumbuliwa na maradhi pia.

Katika uhai wao mama alikuwa ni dalali wa kununua na kuuza maeno wakati baba alikuwa anamiliki studio yake ya picha.

Mtoto wao wa mwisho Daniel anasema mama yake kila mara alikuwa anasema hapendi kuja kushuhudia mumewe akifa na kumuacha peke yake huku baba yake nae akisema hawezi kuishi bila mkewe!

0 Maoni:

Toa Maoni