Aliyejibadili jinsia kuwa mwanaume ajifungua kidume

Kwa mara ya kwanza huko barani Ulaya mtu ambaye alibadili jinsia akabeba ujauzito kwa njia ya kupandikizwa kwa mbegu za kiume amejifungua.

Mtu huyo ambaye hakutajwa jina alizaliwa akiwa mwanamke kabla ya kuamua kujibadili jinsia na kuwa mwanaume amejifungua mtoto wa kiume nyumbani kwake huko Berlin nchini Ujerumani.

Mwanaume huyo amesisitiza kuwa aliamua kujifungulia nyumbani kwasababu hakutaka kutajwa kama mama kwenye nyaraka yoyote ya hospitali inayotakiwa kisheria nchini humo.

0 Maoni:

Toa Maoni