Mchungaji ataka kuuza mtoto aliyezaa na muumini wake

Mchungaji maarufu wa nchini Nigeria amekamatwa na Polisi wa jimbo la Imo kwa madai ya kutaka kushirikiana na mtu mwingine kumuuza mtoto wa mpenzi wake kwa fedha ya Nigeria Naira 100,000.

Mchungaji alimwambia mama wa mtoto huyo kuwa mtoto amefariki kwenye mtaa wa Ajiwe,kwenye jimbo la Aba.

Kamishna wa Polisi wa jimbo la Imo, Mohammed Katsina amesema mchungaji huyo anayesifika jimbo la Imo anayeishi Avutu Obowo, alimpa ujauzito muumini wake ambaye ni mpenzi wake.

Mdada huyo inaelezwa kuwa alikuwa yupo kwenye maumivu ya kujifungua wakati mchungaji alipomuita mwanamke mwingine aliyekwenda kumtambulisha hospitali inayoitwa Angel of Mercy ambako ndipo mpenzi wake alijifungulia.

Taarifa hii imekuja huku ikiwepo taarifa ya mchungaji wa Coza Ministries kutuhumiwa kuwa na mahusiano na waumini wake wawili madai yaliyosababisha mke wa mchungaji huyo kutafuta huduma ya maombi.

0 Maoni:

Toa Maoni