Watoto wapata watoto tena mapacha watatu!!

Katika hali ya kushangaza binti mdogo mwenye umri wa miaka 14 Mwanaharabu Wamukoya  kutoka katika kijiji cha Harambee nchini Kenya amejifungua watoto mapacha watatu wiki iliyopita!
Mwanaharabu na watoto wake
Huku kukiwa na mshangao bado,imefahamika baba wa watoto hao ni mwanafunzi wa sekondari mtoto mwenye umri wa miaka 16 ambaye hajulikani alipo kwa sasa baada kwa kuogopa mkono wa sheria na majukumu pia.

''Mpenzi wangu hana uwezo wa kunihudumia mimi pamoja na watoto,hata hivyo naishukuru serikali kwa kuweza kugharamia fedha za hospitali nitaweza kutoka huru bila kudaiwa chochote'' alisema mtoto huyo.

Kwa mujibu wa nesi aliyekuwa katika zamu Mary Marumbu mama na watoto wake wako salama tayari kurudi nyumbani na kesi ipo polisi.

Kwa mujibu wa ripoti,Kenya ina namba kubwa ya watoto wanaopata mimba kwa Afrika mashariki.

0 Maoni:

Toa Maoni