Ukaribu uliokuwepo kati ya msanii wa Filamu Tanzania Dr. Cheni na mwigizaji mwenzake Elizabeth Michael a.k.a Lulu umeibua maswali mengi sana kwa watu huku kukiwa na tetesi kuwa wawili hao ni wapenzi.
 |
| Dr. Cheni katika studio ya Times fm |
Hatimaye leo kupitia Kipindi cha
Hatua Tatu cha
Times fm Dr. Cheni amefungukia uhusiano wake na Lulu na kusema amekuwa akisikia maneno mengi mtaani watu wakimtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Lulu lakini ukweli ni kwamba hakuna kinachoendelea katika yao zaidi ya kuwa mstari wa mbele kumsaidia alipopatwa na matatizo na kuwekwa rumande kama binadamu.
 |
| Team Hatua Tatu Mie,Mkisi na Dr Cheni studio leo |
Akiendelea kufunguka Cheni amesema anawashangaa watu wanaozusha mbona alishawahi kumsaidia msanii mwenzake Cloud alipopata matatizo na alikuwa mstari wa mbele kwenda polisi,kumpelekea chakula n.k lakini hakuna aliyesema lolote kwamba atakuwa na mahusiano na dada wa Cloud au nini iweje kwa Lulu wazungumze!
Habari nyingine kutoka kwa Dr. Cheni ni kuwa anatarajia kutoka na filamu mpya itakayoitwa
Nimekubali kuolewa huku kwenye cover ya mbele itaonekana picha yake mwenyewe akiwa katinga shela na chini ya picha hiyo kuna maandishi
kwa hiyari yangu, kwa hiyo ni
Nimekubali kuolewa kwa hiyari yangu..kaa tayari kwa burudani.
0 Maoni:
Toa Maoni