Dunia ina mambo..utaamini huyu bidada alikuwa dume!

Anaitwa Titica..alizaliwa kwa jina la Teca Miguel Gracia ni muimbaji na mchezaji ambaye anafanya yake huko Angola. Alibadili jinsia yake na kuwa mwanamke miaka minne iliyopita baada ya kufanyiwa operesheni nchini Brazil.

''Ahsante Mungu nina furaha sana sasa,imenichukua muda mrefu na mlolongo mrefu pia pamoja na kujitolea lakini ahsante Mungu kila kitu kinaenda vizuri'' amesema Titica

Akiwa na miaka 26 sasa Titica ni sura mpya ya kipeke Angola kwenye muziki katika style maarufu ya Kuduro na kuelekea mafanikio Siku chache zilizopita shirika la UNAIDS walimfanya kuwa balozi wao.

Ukiachana na mengine,Titica bado ana mashabiki wachache na wengi wa hao wakionekana kupenda muziki wake zaidi ya mambo yake ya kujibadili jinsia.

0 Maoni:

Toa Maoni