Kisa cha kusikitisha cha mtoto aliyefariki kwa kutengwa sababu ya maradhi!

Mtoto Mwajuma mwenye umri wa miaka 16 aliyekuwa katika mateso makali kutokana na ugonjwa wa ajabu unaomsumbua amefariki dunia.

Mtoto huyo ambaye ni mzaliwa wa Bagamoyo mkoa wa Pwani, alikuwa anasumbuliwa na tatizo la kusinyaa kwa mwili huku mwili mzima ukiandamwa na vidonda.
Mwajuma wakati kalazwa Muhimbili
Akizungumza na mwandishi wetu, mama wa Mwajuma alisema kuwa mtoto wake kabla ya mauti kumkuta alianza kusumbuliwa na tatizo hilo kutokana na yeye kumuacha ndani wakati akiwa mdogo na kwenda kwenye vibarua kwa ajili ya kujipatia pesa ya kujikimu.

"Nilikuwa namuacha kwa muda mrefu sana Mwajuma ndani hata kwa saa kumi na nilikuwa nikimuacha anajisaidia hata mara tatu bila kubadilishwa huku akilia kwa muda mrefu sana na ndipo alipoanza kupatwa na maradhi hayo yaliyoendana na utapiamlo," alieleza mama Mwajuma.
Mama yake na Mwajuma akiwa hospitali
Mwajuma ambaye alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi ya watoto Makuti B, hali yake ilikuwa si yakuridhisha kiasi cha kupelekea kifo chake.

Mama huyo wa Mwajuma katika mahojiano na mwandishi wetu Edson Mkisi Jr alisema ndugu wote wamemtenga kutokana na tukio hilo huku wengine wakidai maradhi ya mtoto huyo ni uchuro kwenye ukoo huo.
Mwandishi na mtangazaji kutoka Times fm Edson Mkisi Jr akiwa kwenye mahojiano
"Baadhi ya ndugu hawataki hata kunisikia na walikuwa tayari mtoto afe wasema ni uchuro kwenye familia,na tangu nifike hapa Muhimbili hakuna ndugu aliyewahi kunitembelea hata kwa kuja tu kumuangalia mtoto ama kuniletea chakula zaidi ya wasamaria wema na hapa Hospitalini," alisema mama Mwajuma.

0 Maoni:

Toa Maoni