Muziki na shule: Rapper M Rap kurudi shule tena!

Rapper kutoka B Hit’s Music Group Richard Prudence aka M Rap Lion ameanza rasmi kujifunza mafunzo ya elimu ya Chuo Kikuu akichukua masomo ya 'Bachelor Of Insurance and Risk Management' kwenye chuo cha Biashara 'IFM' kilichopo maeneo ya Posta Jijini Dar es Salaam.

M Rap Lion amesema tayari ameshaanza kujifunza masomo ya elimu ya chuo Kikuu katika Chuo cha IFM kilichopo Jijini Dar es Salaam,kuhusiana na muziki alisema atapanga ratiba maalumu ya kuweza kuvimudu vyote viwili kwa wakati mmoja.

''Tayari nimeanza elimu ya Chuo Kikuu pale IFM nikichukua Bachelor of Insurance and Risk Management 'Course'ambayo yanahusiana na mambo ya BIMA,ambayo inalenga kuhudumia na kulinda usalama wa mali za kila Mtanzania kwa lugha ya kigeni naweza fupisha kwa kusema 'SOCIAL PROTECTION' kwani kila siku matatizo huwapata wananchi ambao wengine nyumba zao huungua na hata magari kupata ajali ikiwa yana BIMA nilichaguliwa 'TUMAINI UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM' lakini kutokana na sababu tofauti ilinibidi nichague Chuo kingine ambacho hicho nimeanza sasa,na kuhusu muziki wangu nitaendelea kufanya kama kawa ila nitapanga ratiba nzuri ya kuweza kuvimudu vyote viwili ili nisipoteze mashabiki wangu ''Alisema M Rap Lion.

Habari kwa hisani ya Website ya Times fm.

0 Maoni:

Toa Maoni