Picha aliyopost Kim Kardashian katika mtandao ikimuonyesha ana kivazi cha kuogelea tu na kuzua gumzo imempa kiburi rapper Kanye West cha kutamka hadharani kuwa wao ndio couple ambayo inafunika zaidi kwa mitindo ya mavazi na kwamba wana ushawishi hata zaidi ya couple iliyoko White House, yaani Barack Obama na mkewe Michelle!
Moja kati ya kigezo alichotumia Kanye West kumpandisha juu Kim Kardashian zaidi ya First Lady wa U.S.A Michelle Obama, eti ni kwa sababu Michelle hawezi kupost Instagram picha akiwa amevaa bikini kama anavyofanya Kim K.
Yeezy alifunguka katika interview aliyofanya na Ryan Seacrest, October 29.
“Kiujumla, sisi ndio wenye ushawishi mkubwa zaidi kwa sababu ni kweli, hususani kwa mavazi. Hakuna mtu anaetazama kipi (Barack Obama) anavaa. Michelle Obama hawezi kuweka picha Instagram (akiwa amevaa bikini) kama ile ambayo msichana wangu aliweka siku ile.” Alijigamba Kanye West.
Hakuishia hapo, aliendelea kumwagia sifa mama mtoto wake na kusema yeye ndiye anaestahili kukaa kwenye cover ya jarida maarufu la Vogue kwa kipindi hiki.
Hakuishia hapo, aliendelea kumwagia sifa mama mtoto wake na kusema yeye ndiye anaestahili kukaa kwenye cover ya jarida maarufu la Vogue kwa kipindi hiki.

0 Maoni:
Toa Maoni