Unajifunza nini kutokana na kisa hiki?

Najua unaweza kuwa ulishasoma hiki kisa kwenye mitandao huko lna ukasoma lakini mimi pia nimevutiwa na kuguswa pia na nimejifunza kitu hapa..hebu na wewe soma halafu uniambia umejifunza nini kutokana na story hii..


Anachokifanya anti hapo pichani, si kigeni, anatengeneza chapati. Anti huyu huamka saa kumna1 asbuhi, akoke moto, akande unga, atengeneze chapati, akaange. Hii ni kazi yake ya kila siku. Anti huyu amekuwa akipika chapati miaka mi5 sasa, hivyo hivyo akiziuza kwa shida, maana kinachofuatia hapo ni kusubiri wateja, chapati moja TSH 200/=. Bahati, hapo jirani yake akahamia mdada mmoja, akawa mteja wake, anachukua chapati mbili kila siku anaenda nazo kazini. 

Mara yule mdada akaanza chukua nne, mara 8 mara 10, mara akaweka oda ya chapati 100 kila siku. Mama akawa hana jasho la kuuza tena, yaani dada wa watu akifika tu analamba chapati 100 anasepa. Kwa vile anachukua 100, mdada akaomba awe anauziwa moja kwa 150/=, anti akaona inalipa, anti akakubali, mdada sasa akawa anachukua chapati 200 kila siku. 

Mama wa watu akaanza fuatilia kisirisiri, mdada anapeleka wapi? Kumbe yule dada anazichukua, anaenda nunua foil, anazifunga kwenye foil anauza Ofisini kwao na ofisi ya shosti yake jirani. Anauza moja Mia Tano. 

Mama kugundua, kaanza vimba, mara ananuna nuna, mara siku nyingine atengeneze 40 tu, mara aseme leo nnaumwa, mara leo nna oda kubwa dadaangu siwezi kukupa, basi akendelea hivyo ili mdada ashindwe. 

Mdada akamwambia anti naona mie niache tu. Anti akafurahi. Kesho yake anti akatengeneza 200 akamtuma mtoto wake wa kike akaziuze ktk zile ofisi mbili, unajua nini, aliuza 10 tu. Yule mdada alishaangaliaga plan B, anachukua kwa mama mwingine, tena anazipata kwa mia mia, sasa ana ofisi ya 3 anasaplai chapati 300 kila asbuhi. Kwa huyu mama mwingine jiko halikuwa zuri akampa jiko zuri na hotpots.


Tujifunze:

1. Ukiuza Simu yako laki, aliyenunua akaenda uza milioni, piga kimya, haikuhusu!

2. Ukiona mwenzako kafanikiwa kwa kufanya kitu fulani, usidhanie basi nawe unaweza kufanikiwa kwa kitu kilekile kama yeye hujui nini siri ya mafanikio


3.Jifunze kutokana na mafanikio ya mwenzako sio kukasirika na kuweka bifu

4.Dada alishuhudia mwenzake akitumia foil kuweka chapati na kuuza ofisini yaani inavutia kununua kutokana na vifaa vinavyotumika so ilibidi nae abadilike na kuwa kidijitali zaidi..nadhani umenielewa!

0 Maoni:

Toa Maoni