Unakumbuka sakata la dada wa kazi aliyezaa na Mahita? Azua jipya tena!

Mfanyakazi wa ndani aliyedaiwa kuzaa na aliyewahi kuwa Mkuu wa Jesho la Polisi Nchini ambaye kwa sasa amestaafu Bw. Omari Mahita, Rehema Shaaban maarufu kama Mama Mahita, hivi karibuni alijikuta akitupiwa vyombo vyake nje katika nyumba aliyokuwa amepanga kutokana na kile kilichodaiwa kushindwa kulipa kodi ya nyumba kwa wakati!

Wakitikisa taya na Mwandishi wetu, Edson Mkisi Jr wa Blog hii, mashuhuda walisema mama huyo tangu kuamini kwenye nyumba hiyo maeneo ya Mwananyamala Kisiwani, amekuwa mtu wa vituko kwa majirani zake kiasi cha kuwa na vitisho vya kuwapeleka mahakamani bila sababu za msingi.

Baadhi ya majirani walioomba hifadhi ya majina yao walisema mama Mahita, amekuwa mchonganishi huku akijinadi kutomuogopa mtu kwa sababu ya kuzaa na Mahita.
"Huyu mama nahisi kabisa atakuwa hayupo vizuri kiakili, anaweza kukaa akagombana na wewe halafu anakwambia hakuna mtu ninae muogopa hapa mtaani kama nilimshinda Mahita nani ataniweza na lazima niheshimiwe mimi ni mke wa mtu mkubwa Tanzania," alisema jirani mmoja.

Wakizungumzia sababu ya kutimuliwa kwenye nyumba aliyokuwa amepanga eneo hilo, mashuhuda hao walisema mama huyo amekuwa akijinadi na kutangaza kwa watu kwamba nyumba alnayoishi amenunua kwa milioni 12!Walisema hilo ndilo lililomkera mama mwenye nyumba wake na kuamua kumtimua ndani ya nyumba hiyo."Sasa kwasababu alitangaza sehemu kubwa ya eneo hili huku akidai pesa hizo alilipiwa na Mahita ndio anaona aibu kuhama sasa ingawa serikali ya Kata amemtaka kuondoka kwenye nyumba hiyo".

Akizungumza na mwandishi wetu, mama mwenye nyumba hiyo aliyejitambulisha kwa jina mola la Aisha alisema mama Mahita amekuwa mtu wa matatizo ndani ya nyumba yake kila kukicha kiasi cha kutangaza kwa watu amenunua nyumba hiyo. Aliongeza kwamba mbali na kituko hicho, mama huyo amekuwa akimtishia kwamba atamuonyesha eti kwa sababu alizaa na Mahita.

Mama Mahita alipotafutwa na Blog hii katika kupata ukweli wa sakata hili toka kwake, alisema hawezi kuzungumzia tukio hilo kwa sababu amelala. Hata Hivyo, asubuhi yake alipotafutwa mama Mahita hakupokea simu yake mara zote alizopigiwa.

0 Maoni:

Toa Maoni