UNYAMA : Mtoto alazimishwa kuishi kwenye buti ya gari kwa miaka 2!

Katika hali isiyo ya kawaida mtoto mdogo wa kike amelazimishwa na wazazi wake kuishi kwenye boot ya gari kwa miaka miwili.

Hiyo imetokea nchini Ufaransa na wachunguzi wanasema mtoto huyo alikutwa akiwa mtupu bila nguo na mafundi mekanika(Mechanics)ambao walikwenda kwenye familia hiyo kwaajili ya kutengeneza gari aina ya Peugeot 307.

Mafundi hao waliwapa taarifa polisi uwepo wa mtoto baada ya kusikia sauti ngeni ya manungúniko kutoka kwenye gari hiyo.

Mama wa mtoto huyo mwenye miaka 45,raia wa Ureno aliyefahamika kwa jina la Rose-Marie,alisema sauti hiyo inatoka kwenye mdoli lakini lilipofunguliwa boot la gari hiyo akakutwa mtoto mdogo akiwa uchi.
Garage alipokutwa mtoto

Mama wa mtoto huyo akatakiwa kumpa chochote cha kula mtoto huyo ambaye alionekana pia kusumbuliwa na njaa kabla ya wataalamu wa tiba kufika kumchukua na kwenda naye hospital kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Mtoto huyo yupo chini ya uangalizi wa Ustawi wa jamii wakati huu ambapo wazazi wake wanatuhumiwa kwa kosa la unyanyasi wa watoto na kama ikithibitika wanaweza kuhukumiwa kwa kifungo cha miaka 10.

0 Maoni:

Toa Maoni