Davido hana hofu..asema hana mpinzani!

Kutoka nchini Nigeria mkali wa songi linalofanya vizuri kwenye radio na televison Skelewu,Davido amefungukia mafanikio aliyonayo na kuanika kuwa hana hofu na yeyote katika soko la muziki.


 ''Simuhofii yoyote hata Wizkid,hizo ni tetesi tu..Mungu yuko na mimi,huwa naingia studio,nafanya muziki na kila kitu kiko sawa.Siogopi ushindani kwa sababu huu ni muziki anaweza kuja mtu na kufanya vizuri na kungáa na kuwa na mashabiki. Nna mpango wa kujiingiza kwenye biashara ya mafuta na gesi na kaka yangu mkubwa.Nataka kufanya muziki kwa miaka 10 kwa muda huo ntakuwa na miaka 30.Umaarufu katika umri mdogo ni nyongeza kwa sababu nna miaka 10 mbele ya ushine wakatiki kuna watu wanaanza wakiwa na miaka 29-30" Alifunguka Davido

Akizungumzia wimbo wake wa Skelewu anasema an video tatu ambazo ziko hewani na anafanya video kama filamu so unaweza kuangalia yoyote utakayopenda na kama hamna uliyopenda anaweza kutengeneza nyingine tena maana ni rahisi!

0 Maoni:

Toa Maoni