'Mama mchungaji' ammwagia maji ya moto mdogo wake kisa mapapai!

Polisi wa Lagos nchini Nigeria wanamshikilia mwanamke mmoja ambaye ni mke wa mchungaji Mrs. Angela Uzoma (28) kwa kosa la kummwagia maji ya moto mdogo wake.

Mwanamke huyo amemwagia maji ya moto mdogo wake wa kike Chidinma Chukwu mwenye umri wa miaka 14 na kumsababishia majeraha makubwa kisa kikiwa ni kuuza mapapai machache aliyopewa kutembeza siku hiyo na kurudisha mengine ndipo mwanamke huyo alipopatwa hasira na kutoa adhabu hiyo!

Cheki binti huyu mdogo alivyoharibiwa kisa mapapai!
 Baada ya Angela kumuunguza mdogo wake alijaribu kuficha ajali hiyo kwa kukataa kumpeleka hospitali badala yake akatafuta nurse wa kumtibia nyumbani lakini Mungu mkubwa msamaria mwema alijitokeza na kwenda kuripoti polisi ndipo mwanamke huyo akatiwa mbaroni.

Baada ya kuswekwa rumande bidada huyo alijitetea kuwa shetani alimpitia na anaomba wayamalize mambo hayo yasifike mahakamani huku mumewe ambae ni mchungaji akisikitishwa na kitendo cha mkewe na kusema ameenda mbali sana!

0 Maoni:

Toa Maoni