Mwanaume mwenye mvuto zaidi ametajwa...huyu hapa!

Jarida la People limemtaja member wa kundi la Maroon 5 Adam Levin kama mwanaume mwenye mvuto zaidi aliye hai ‘Sexiest Man Alive’.

Adam Levine ambaye pia ni coach wa shindano la kuimba la ‘The Voice’ amewekwa kwenye jarada la jarida hilo litakalotoka rasmi ijumaa (November 22). 
 
Akiwa ni mtu wa tano kupewa title hilo na jarida hilo baada ya Channing Tatum, Bradley Cooper, Ryan Reynolds na Jonny Depp, Adam amesema hakutarajia kitu kama hicho na kwamba hata aliposikia kwa mara ya kwanza alidhani walikuwa wanatania lakini mwisho wa siku aliamini haikuwa utani.

“Kama mwanamuziki, unakuwa na ndoto kuwa unataka kushinda Grammys, lakini sikudhani kama hiki kiko mezani. Nilishangazwa na ilionekana kama walikuwa wanatania, lakini hawakuwa wanatania, so that’s cool.” Adam aliliambia jarida hilo.

Hata hivyo kumekuwa na utata katika kutoa mataji haya kwa kuwa mtazamo wa wengi huwa ni kwa nini wapewe watu maarufu tu? Lakini inawezekana kuwa kwenye spotlight ikawa sababu inayopelekea wao kuonekana zaidi.

Lakini kama sababu itakuwa hiyo, basi wengine hushauri ingekuwa “mwanaume maarufu mwenye mvuto zaidi.” Ni mitazamo.!
Habari kwa hisani ya website ya Times, www.timesfm.co tz.

0 Maoni:

Toa Maoni