Kijana huyu aliwahi kuzawadia gari la aina ya Toyota Corolla na safari za kwenda nchini China na Dubai zilizolipiwa kila kitu. Pia walikuwa wakiishi pamoja kwenye jumba la kifahari la mume wa mwanamke huyo huku mambo yakionekana kwenda shwari mpaka mwanamke huyo alipozua janga hilo kwa kutaka waachane sababu ikiwa ni kwamba mumewe anarejea kutoka ulaya alipokwenda.
Kama kawaida habari hii haikupokelewa vyema na Michael ambaye alitishia kujiua kama itatokea kuachana na mwanamama huyo na kwenda mbali zaidi baada ya kujiua kweli na kabla ya hayo inasemekana ugomvi mkubwa sana ulitokea baina yao.
Inasemekana kwa mujibu wa Michael hakutaka kushuhudia au watu kumuona akirudi kwenye maisha yake ya kimaskini baada ya bata alizozoeshwa!
Jamani fanyeni kazi kwa bidii acheni kutegemea mali za kuhongwa ambazo mwisho wa siku zinawagharimu na kufanya maamuzi ya ajabu kama ya kijana hapo!


0 Maoni:
Toa Maoni