Akielezea kuhusiana na gauni hilo Denrele ameandika kuwa Goldie alipanga kutinga kivazi hicho katika tuzo zilizopita za zilizopewa jina la African Magic Viewers Choice Awards lakini Mwenyezi Mungu akawa na mipango yake mingine so hakuweza kulivaa baada ya kufariki kabla ya tuzo hizo kufanyika.
Cheki baadhi ya picha za gauni hiloa mbalo mwenyewe ameelezea kuwa ilibidi atinge na suruali ya dada yake ili angalau kunogesha maana yeye ni mwanaume.
Denrele na Goldie pia walikuwa na mpango wa kuanzisha Reality tv show ambayo ingebeba jina la True Friendship ambayo ingeonyesha maisha yao ya kila siku lakini wakati wako kwenye mipango ndio mwenyezi Mungu akamchukua.



0 Maoni:
Toa Maoni