Akizungumza katika mahojiano maalum na mwandishi wetu Edson Mkisi Jr, Shariff alisema alikuwa akiishi nyumba hiyo kwa msaada ya AT kutokana na jinsi alivyokuwa akimsaidia kwenye shughuli zake za muziki.
"Kutokana na jinsi nilivyokuwa nikimsaidia kwenye nyimbo zake mbalimbali AT aliamua kunipangia nyumba nzima kule Kijiwe Samli lakini cha kushangaza baada ya kunilipia mara kadhaa lakini dakika za mwisho alianza kusita kulipa na hadi kufikia deni la laki tisa,sasa kibaya zaidi yule mwenye nyumba anayenijua ni mimi kwa sababu ndio niliyekwenda kupanga si AT sasa adha yote na fedheha zinakuja kwangu na AT nikimpigia simu hapokea wala ataki kujibu meseji zangu!" alibainisha.
Alisema lengo la kwenda kwenye vyombo vya habari ni kujua jinsi ya kumpata AT ili aweze kulipa deni hilo.
Baada ya kupata taarifa hizo mwandishi wetu pia alimtafuta msanii kwa lengo la kusikiliza upande wake sanjari na kumpa haki yake ya msingi ambapo katika majibu yake AT alisema hamjui mtu huo na kwenda mbali zaidi kwa kudai kwamba anatafuta 'kick' kupitia jina lake.
"Mimi huyo mtu simjui kabisa sina mjomba kama huyo kama unabisha nikupe namba ya mama yangu umuulize kama mimi ninamjomba wa namna hiyo,huyo jamaa atakuwa anatafuta kick tu ya kuenesha maisha yake hapa mjini lakini mimi simjui hata kidogo," alisema.
AT aliongeza kwamba kama mganga huyo kweli ni mganga afanya kazi ili yeye apotee kimuziki kama kweli yeye ndiye aliyemfikisha hapo alipo sasa.
Msikie hapa AT anavyozungumza na mganga
Hapa sangoma huyo akafunguka baada ya AT kusema hamjui.

Kweli huyo mganga anatafuta kiki na mbona hiyo sauti ya kwanza si ya at ama kweli mjini kuna mambo
ReplyDelete