Beyonce abebeshwa tuhuma nzito za 'kubanjuka' na rais Obama!


Mwanadada mrembo mke wa Jay Z,mwanamuziki mwenye sauti tamu na mvuto Beyonce amekumbana na uzushi wa hali ya juu baada ya habari kusambazwa na mtandao wa mmoja kutoka Ufaransa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na raisi wa Marekani Barrack Obama!

Kuna mgongano wa habari kati ya baadhi ya vyombo vya habari vya Ufaransa na vile vya Marekani kuhusu uhusiano uliopo kati ya Beyonce Knowles na rais wa Marekani, Barack Obama.

Gazeti la Ufaransa la Le Figaro liliripoti kuwa kuna uhusiano wa siri wa kimapenzi kati ya rais wa Marekani, Barack Obama na mwimbaji ambaye ni rafiki wa karibu wa familia ya Obama, Beyonce Knowles.

Habari hizo zilishindiliwa msumari na mpiga picha Mfaransa Pascal Rostain, ambaye ni rafiki wa mke wa rais wa zamani wa Ufaransa, Carla Bruni, aliyelieleza gazeti hilo kuwa habari hizi hivi karibuni zitaandikwa na waandishi wa habari wa Marekani na inaweza kuwa kama ile scandal iliyomtesa Bill Clinton, kuhusu Monica Lewinsky (1995/1996).
“Kuna kitu kikubwa kinachoendelea kati ya wawili hawa, tusisahau Marilyn (Monroe) au Monica Lewinsky. Unaweza kuwa rais wa nchi ya kwanza yenye nguvu duniani…hiyo haikufanyi usiwe mwanaume kamili.” Rostain aliliambia gazeti hilo.

Hata hivyo, ingawa Rostain alidai kuwa Washington Post lingeandika habari hiyo leo (February 11), Washington Post imeandika habari tofauti kabisa huku baadhi ya waandishi wakikanusha habari hizo.
“Sio kweli hata kidogo”, msemaji wa Post Kris Coratti ameiambia Poynter.com kwa njia ya barua pepe.
Naye mwandishi wa wa New York Times, Dave Itzkoff ametweet kuhusu tuhuma hizo na kuonesha kutokubaliana kabisa na kilichoandikwa na gazeti la Ufaransa.


Ni habari zilizosambaa kwa kasi na kushtua watu wengi kwa kweli.. Mama Ivy Blue na Obama!

0 Maoni:

Toa Maoni