Majanga ya kina dada na mavazi ya kihasara..


Hebu angalia huyo dada aliyeinama hapo jamani! Mwili wake na alichovaa kisha akainama kabisa
Wanawake tumekuwa tukidai kupewa heshima pia tumekuwa tukilalamikia vitendo vya udhalilishaji tunavyofanyiwa ikiwa ni pamoja na kuzomewa na kuvuliwa nguo pindi tunapovaa vinguo vya kihasara lakini sisi wenyewe tumekuwa tukichangia hayo yanayotupata.

Sasa hivi ni kawaida kabisa kukutana na wanawake wametinga vivazi vya kihasara hata mchana bila hofu huku wakijichetua na kujitundika kwenye mitandao ya kijamii bila haya.Hivi kwa mfano wa vivazi nilivyovionyesha kwenye picha hapo nani atakuheshimu hata kama wewe ni nani sijui huko?

Wengine hata hawajiangalii maumbile yao na nguo wanazovaa badala ya kupendeza wanageuka kichekesho mbele za watu kisa nao wanataka kwenda na fasheni! Wewe unajijua una mwili mnene na minyama halafu unavaa nguo inayokuonyesha mpaka sehemu zako za siri zilivyokaa sasa hapo heshima utapata wapi na saa ngapi?
Huyu nilikutana nae Dar Live hapo alikuwa kalewa hoi halafu anajifunua na kukata mauno mbele ya wanaume... Na huo mwili wake na anachokifanya ni huruma
 Kama kweli wanawake tunataka heshima basi tujitambue sisi ni nani na tuna nafasi gani katika jamii. Yangu ni hayo tu kwa leo.
Ni nini hiki?

1 comment: