Kasisi mmoja wa kanisa katoliki mwenye umri wa miaka
85 amekiri kosa la kulawiti watoto wengi pamoja na kuwatendea unyama
watoto wengine wasichana baada ya kufukuzwa kutoka katika kisiwa cha
Tenerife nchini Uhispania.
Katika kesi iliyokuwa iliyosikilizwa katika mahakama mjini London kasisi huyo, kwa jina Francis Paul Cullen, alikiri makosa 21 ya kuwatendea uchafu watoto saba.
Vitendo cha kuwalawiti watoto wavulana na kuwatendea unyama wasichana, vilitokea kati ya mwaka 1957 na 1991.
Msemaji wa dayosisi ya Nottingham mjini
Uingereza kasisi Andrew Cole alisema kuwa amefurahi kwa kasisi huyo
kukiri makosa dhidi yake.
Kasisi Cole alisema kuwa hakuna kinachoweza
kuondoa masaibu yaliyowatokea watoto lakini kasisi Cole alisema anatumai
kuwa hii itawasaidia kwa njia moja au nyingine.
Cullen atahukumiwa tarehe 24 mwezi Machi.
Alifanya kazi kama kasisi katika dayosisi
Mackworth parish ya Christ the King katika mtaa wa Derbyshire kati ya
mwaka 1960 na 1978.
Alihamia katika kanisa ya Buxton kuanzia mwaka 1978-87 na kanisa nyingine ya Hyson Green, kati ya mwaka 1988-91.Alistaafu Septemba mwaka 1991.

0 Maoni:
Toa Maoni