Dunia ina mambo! Mwanadada mwenye vituko kutoka nchini Kenya Huddah Monroe ametoa kali ya mwaka aliposema siku za baadae atakapokuwa na familia atawapa Google pesa ili wafute picha na video zake chafu kusudi mtu anapotafuta asiweze kuziona tena..kifupi ibaki stori tu!
Akifanyiwa mahojiano kwenye kituo cha televisheni cha nchini Kenya KTN na mtangazaji Mwanaisha Chidzuga ndipo alipoulizwa kuwa picha na video za utupu na zisizo na maadili anazotupia kwenye mitandao ya kijamii kila kukicha haoni kama zitaleta madhara baadae atakapopata familia na watoto? Akafunguka ''Unajua money can buy everything na pesa ni kila kitu... kipindi hicho nitakuwa na pesa,nitawapa Google hela ili wafuta historia yangu yote so hawataiona hakuna linaloshindikana..''
Katika mahojiano hayo pia aliongozana na rapa kutoka Kenya Colonel Mustapha ambapo walitoboa kuwa wana uhusiano wa kimapenzi japo walichukua muda kulithibitisha hilo kutokana na kupata kigugumizi cha ghafla!
Cheki mahojiano yao hapa.

0 Maoni:
Toa Maoni