Imani yamponza Mchungaji,auliwa na nyoka wake mwenyewe!


Mchungaji wa kanisa la Pentecostal Full Gospel Tabernacle in Jesus Name Jamie Coots,anayefahamika kwa kuhubiri akiwa na nyoka aliyejiviringisha mkononi amepoteza maisha baada ya mmoja wa nyoka hao kumng'ata.

Mchungaji Coots, kabla ya kifo chake alikuwa pia kwenye show ya Tv inayoitwa National Geographic reality show akielezea kuhusiana na uhubiri kwa kutumia nyoka huyo akisema waumini wa kikristo waliagizwa na Yesu kristo kwenye Marko 16:15-18.

Sehemu ya mstari huo inasema :
"Ishara hizi kwa wale waaminio katika jina langu zitawaongoza kuondoa mapepo na kunena kwa lugha mpya,wakinywa kinywaji chochote chenye sumu hakitawadhuru na wakiweka mikono yao kwa wagonjwa watapona"
Kupitia neno hilo Pastor Coots anahubiri kuwa wote waaminio watalindwa wanaposhika nyoka lakini hali ikawa tofauti wakati mchungaji huyo aliposhambuliwa na nyoka huyo Jumamosi iliyopita wakati akihibiri mbele ya waumini wa Kentucky.

Haraka huduma ya dharura walikimbilia kanisani kwake kumpatia matibabu lakini wakakuta amerudi nyumbani kwake na walipokwenda akawafukuza akikataa matibabu kwasababu ya imani yake.

Saa moja baadaye Pastor huyo akafariki.
















Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi!

0 Maoni:

Toa Maoni