![]() |
| Ndege binafsi anayomiliki Jaguar 'Air Jaguar' |
Msanii anayedaiwa kuwa na utajiri mkubwa kuliko wasanii
wengine nchini Kenya, Jaguar anazidi kupanda ngazi za mafanikio kupitia
muziki wake baada ya kusaini deal nono na kampuni ya MTech Kenya
itakayokuwa na jukumu la kusambaza kazi zake Afrika.
Menejimenti ya Jaguar, imeiambia Red Pepper Online kuwa msanii huyo
alikuwa anaangalia katika kutanua fan base yake Afrika Magharibi na
Kusini na kwamba MTech ambao wanapatikana huko na wanaushawishi walikuwa
watu sahihi wa kufanya nao kazi kwa kuzingatia lengo lake.
Baada ya kusaini mkataba huo na MTech, Jaguar anatarajiwa kuingia
studio kufanya kazi na rapper wa Naija ‘Ice Prince’ ambaye alishinda
tuzo ya BET.
Jaguar anaungana na P-Unit, Wyre, Radio & Weasel, Keko wa
Uganda, Victoria Kimani, Ice Prince, P Square, Flavour, J Martins,
Brackets Eko Dida na wengine ambao wanafanya kazi na MTech.
Habari kwa hisani ya tovuti ya Times fm.

0 Maoni:
Toa Maoni