Kanye West asababisha Nike iuze mzigo wa viatu vyote kwa dakika 11 tu!


Jina la Kanye West kutokea kwenye toleo jipya la viatu vya kampuni ya Nike ‘The Nike Air Yeezy 2’, limepelekea kampuni hiyo kuuza mzigo wake wote ndani ya dakika kumi na moja, tena kwa njia ya mtandao.

Jumapili, February 9, Kampuni ya Nike iliweka tangazo kwenye akaunti yake ya twitter kuhusu kupatikana kwa viatu hivyo, “The Nike Air Yeezy 2 is now available.” Baada ya tangazo hilo waliweka pia link ya tovuti ambayo ingetumika kununua online viatu hivyo..Cha kushangaza, dakika kumi na moja baada ya tangazo hilo, kampuni hiyo iliandika tweet nyingine iliyodai kuwa mzigo wote umeshanunuliwa, japo hawakutaja ni pea ngapi za viatu zilikuwa zimenunuliwa. “The Nike Air Yeezy 2 has sold out on Nike.com.” ilisomeka tweet ya kampuni ya Nike.


Kwa mujibu wa Daily maily, bei halisi iliyowekwa na kampuni ya Nike ilikuwa $245, lakini kutokana na 'demand' na wingi wa wateja, wateja hao walitoa hadi kiasi cha $ 7,500 kuhakikisha wanapata mzigo huo.
Hata hivyo, hii inaweza kuwa ishara nzuri kwa kampuni pinzani ya Nike (Adidas), kwa kuwa Kanye West alishaweka wazi kuwa ameachana na Nike na ameamua kufanya kazi na Adidas. Hivyo faida hii inaweza kuwa endelevu kwa matoleo ya Adidas yatakayotolewa na kwa kuwa wameshaona jinsi watu wanavyohitaji bidhaa basi watazalisha kwa wingi.

“I took the Adids deal because I have royalties and I have to provide for my family..I’m gonna be the first hip hop designer and because of that, I’m gonna be bigger than Wal Mart.” Kanye West alifunguka katika mahojiano aliyofanya na radio moja nchini Marekani.

0 Maoni:

Toa Maoni