Aliyekuwa mwigizaji maarufu wa Fast & Furious Paul Walker aliyefariki kwenye ajali mbaya ya gari akiwa na rafiki yake Roger Rodas tarehe 30 Nov 2013 ameacha mali zake zenye thamani ya dola milioni 25 kwa binti yake mwenye umri wa miaka 15 huku aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu waliodumu kwa miaka 7 Jasmine akiambulia patupu.
 |
| Paul Walker, Jasmine na binti yake Meadow |
Mwigizaji huyo amemuandika binti yake huyo Meadow Rain Walker kama mmiliki wa mali zote alizoacha huku baba yake Paul Sr akitajwa kama msimamizi.
Paul na mpenzi wake Jasmine walianza mapenzi akiwa na miaka 33 huku msichana huyo alikuwa na miaka 16 kipindi hicho na mpaka anafariki walikuwa pamoja katika uhusiano.
 |
| Aliyekuwa mpenzi wa Paul, Jasmine. Hapa ilikuwa ni kipindi cha msiba ndio alipigwa picha hii. |
0 Maoni:
Toa Maoni