![]() |
| Nisha na mie baada ya kumaliza mahojiano |
Nisha alifunguka hayo nilipofanya nae mahojiano mapema leo katika kipindi cha Hatua Tatu cha Times fm na kumtwanga swali kuhusiana na mafanikio aliyonayo ikiwemo kampuni ya filamu anayomiliki kama ametafuta mwenyewe pesa au kuna baba la baba nyuma ya pazia.
Pamoja na hayo pia amefungukia ishu ya msanii wa bongo fleva Ney wa Mitego na kusema hakuwahi kuwa na mahusiano na Ney,wala hatarajii kuwa na mahusiano na msanii huyo na hayupo kwenye mawazo yake.Amesema hata mpenzi wake anafahamu uaminifu wake kwake na ndio maana habari hizo hazimpi presha.
Nisha amesema ameshangaa kuona kwenye magazeti na kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa amewahi kuwa na mahusiano na Ney na sasa baada ya msanii huyo kuwa na mpenzi mwingine aitwaye Siwema amekuwa akililia penzi la Ney.
Nisha amesema habari za kuanza kuzunguka mahakamani kushtaki kwa kuchafuliwa ni kujipotezea muda wa nenda rudi mahakamani kwaajili ya kufuatilia kesi jambo linalomfanya asifikirie lolote la kushtaki.
![]() |
| Allen Mushi,mie, Nisha na Edwin |
![]() |
| Nisha,Allen Mushi na mie |







0 Maoni:
Toa Maoni