Valentine hii ni uhondo wa kutosha aisee! Kesho usikose kusikiliza Times fm...

Kama wewe ni shabiki na mpenzi wa muziki mzuri wa live band basi Valentine hii itakuwa tamu sana kwako Banana Zorro, Nuruel na wengine wanaounda bendi ya B. Band, siku ya Valentine (Ijumaa, February 14), kuanzia saa tatu kamili hadi saa sita kamili iweke kwenye ratiba yako muhimu ili uisikilize bendi hiyo ikiimba na kupiga Live kupitia kipindi Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm.


Banana Zoro,Stara Thomas,Edson Mkisi Jr na mie studio katika Kipindi cha Hatua tatu
Bendi hiyo itawapa mashabiki burudani kwa muda mfupi itakaokuwa ndani ya studio za Times Fm, na kisha burudani hiyo itahamia ‘Club East 24’ iliyoko maeneo ya Mikocheni, Dar es Salaam kuanzia saa mbili kamili usiku. Kiingilio kitakuwa shilingi 15,000 kwa mtu mmoja na shilingi 25,000 kwa watu wawili (double).

Katika show hiyo iliyoandaliwa na B band kwa kushirikiana  na kipindi cha Hatua Tatu, watakuwepo wasanii wengine wakali akiwemo Stara Thomas, Grace Matata, Maunda Zorro na mwana hip hop Kala Jeremiah aliyeshirikishwa kwenye wimbo mpya watakaouzindua kesho 'you are not alone'.

Zawadi kwa watakaopendeza zitatolewa na watakaofika watapata nafasi ya kuwaimbilia live wapenzi wao huku wakipiwa ala za muziki na B.Band.

MUHIMU: Kutakuwa na comlimentary zitakazotolewa katika kipindi cha Hatua Tatu kesho so niazime tu sikio lako waweza kujipatia yako.

0 Maoni:

Toa Maoni