Anayedhaniwa ana upungufu wa akili akamatwa na ulimi wa binadamu,tuwe makini!

Mwanaume anayedhaniwa ana upungufu wa akili amekamatwa pembezoni mwa barabara huko katika mji wa Ibadan nchini Nigeria akiwa na ulimi wa binadamu pamoja na silaha za hatari!


Sakata hilo limeibuka baada ya simu aina ya Blackberry aliyoificha kulia kwa nguvu hadharani na kuzua taharuki ndipo alipozungukwa na kuanza kusachiwa na hapo akakutwa na vitu vya kutisha kama mkasi,ulimi wa binadamu n.k kitu kilicholeta hasira kwa watu waliotaka kuchukua sheria mkononi bahati nzuri polisi waliokoa jahazi baada ya kufika eneo la tukio na kumchukua.

Jamani tuwe makini na hawa watu wenye upungufu wa akili tunaopishana nao njiani.Nakumbuka nilishawahi kupishana na mmoja kwenye foleni alitaka kufungua milango ya gari na aliposhindwa akaokota jiwe na kuanza kugonga kwenye kioo cha mbele..niliogopaje sasa! bahati foleni ikaanza kwenda ndio ikawa manusura.Wengine ni wazima kabisa kichwani ila tu ujambazi unawasumbua.

0 Maoni:

Toa Maoni