Msako wa ndege ya Malaysia kuendelea,ndugu wapanga kuandamana!

Maafisa wa Australia wametangaza kuwa msako wa ndege ya Malaysia MH370 kusini mwa bahari ya Hindi utarejeshwa tena angalau kwa masaa 24.  

Msako huo ulisitishwa kutokana na hali ya hewa baharini kuwa ya hatari zaidi na kutangaza kuwa ushahidi wa wazi unaonesha kuwa abiria wote wamepoteza maisha na kwamba ndege hiyo imezama baharini.

Wakati Malaysia wakishirikiana kwa ukaribu na Australia wanatangaza hayo, mamia ya ndugu na jamaa wa abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo walioko Beijing wamepanga kukusanyika katika ubalozi wa Malaysia kuelezea hasira na maumivu walionayo juu ya wapendwa wao.

Hata hivyo polisi wamejipanga kuhakikisha hali ya usalama na tayari wamezuia mabasi yanayobeba abiria zaidi ya 300 kutoondoka katika eneo la Beijing hotel ambapo ndugu wa abiria hao wamekaa kwa muda.
Watu hao wameanza kuelekea katika ubalozi huo kwa mguu ili kuhakikisha wanafika katika ubalozi wa Malaysia huku polisi wakiwa wameweka vizuizi.

0 Maoni:

Toa Maoni