Mike Parker amesema imegundulika kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo
kasi usio salama na sio tatizo lolote la kiufundi kwenye gari
walilokuwa wakiendesha.
“Wapelelezi wamegundua kuwa chanzo cha ajali ya gari hilo ni mwendo kasi usio salama katika hali ya barabara hiyo.” Amesema kamanda huyo wa polisi.
Ameongeza kuwa gari hilo aina ya Porsche Carrera GT lilipita katika mitaa ya Santa Clarita, California likiwa na mwendo kasi kati ya kilometa 130 kwa saa na kilometa151 kwa saa, huku kwa sheria ya eneo hilo ilitakiwa liwe na mwendo kasi usiozidi kilometa 70 kwa saa.
Ripoti hiyo imeonesha kwamba Paul Walker na Roger Rodas hawakutumia kilevi cha aina yoyote kabla ya kupata ajali na kwamba walikuwa wamefunga mikanda.
Hata hivyo imeonekana kuwa matairi ya gari hilo yanaweza kuwa yalichangia kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa ya muda wa zaidi ya miaka 9 hivyo yanaweza kuwa yalishindwa kuhimili kwa kiasi fulani mwendo kasi.
November 30, 2013, Paul Walker na Roger Rodas walipata ajali ya gari na kupelekea gari hilo kuwaka moto baada ya kugonga mti.
Paul Walker alitakiwa kuwa kwenye filamu mpya ya Fast and Furious 7 lakini kutokana na kifo chake filamu hiyo ilisitishwa kushutiwa kwa muda.
Watayarishaji wamewatafuta watu wanne wenye maumbo sawa na Paul Walker na wamepanga kutumia teknolojia ya Computer kuhakikisha taswira na sauti ya Paul Walker inapatikana kwenye filamu hiyo kupitia watu hao.

0 Maoni:
Toa Maoni