Baada kupigiwa kura nyingi
zaidi na wasomaji wa gazeti la Ijumaa na hivyo kuibuka mshindi kwenye
shindano la kumtafuta msichana mwenye mvuto zaidi (Sexiest girl)
lililoendeshwa kupitia gazeti hilo,mwanadada Wema Sepetu amewashangaa wanaomponda kuwa hakustahili tuzo hiyo!
Huku akitupiwa picha inayomuonyesha amenyanyua tuzo yake juu kupitia Instagram Wema Alifunguka ya moyoni na kutoa makavu;
Wema alitangazwa rasmi Jumapili (April 20) uwanja wa Dar Live katika
show iliyoandaliwa na Global Publishers. Kwa mujibu wa kura za wasomaji
wa gazeti hilo, Wema aliwafunika Jackline Wolper, Jokate Mwegelo, Nelly
Kamwelu na Elizabeth ‘Lulu’ Michael.
Tamasha hilo la kumtangaza msichana mwenye mvuto zaidi liliambatana na show kali ya kundi la Weusi na kundi la Mkubwa na Wanae.
0 Maoni:
Toa Maoni