Wewe unaesoma hapa ni mwanamke uliyekamilika viungo vyote yaani huna aina yoyote ya ulemavu lakini umekuwa ukilamimika kuwa hupendi rangi yako,pua,mdomo,miguu au hata shepu yako kwa ujumla?? Kama ndivyo basi unamkufuru sana Mwenyezi Mungu! Nataka kukwambia kuwa kuna waliozaliwa na ulemavu ambao hautibiki kwa namna yoyote ile na bado wanaishi kwa kujivunia jinsi walivyo...
Kutana na Lizzie Velasquez msichana mwemye umri wa miaka 25 tu lakini ukimtizama kwa haraka unaweza kuhisi unaomzuia kuongezeka uzito na kumfanya aonekano mzee pia.
Kabla ya watu kujua hilo walikuwa wakimcheka na kumnyooshea vidole kwa sababu ya muonekano wake na miaka michache baadae alitajwa kama Mwanamke mbaya zaidi duniani kwenye video iliyofungiwa sasa. Sasa Lizzie ni rafiki wa celebrities wengi,mzungumzaji anayewatia moyo watu kwa sababu tu hakuruhusu ulemavu wake umuangushe.
Katika mahojiano yake na E alifunguka jinsi alivyopata tabu alipokutana na mtazamo na maoni tofauti kuhusu alivyo,alikuwa anahisi watu walikuwa wakifanya makusudi kuandika vitu vibaya kumhusu ili kumuumiza, lakini sasa kabadiloika na anajivunia tu kuwa alivyo na anajichanganya kama walivyo wengine.
Cheki picha zake alivyo kisha mshukuru Mungu kwa kila alichokujaalia.
Kupia mtandao wa Instagram pia ana zaidi ya followers 90,000 ambao wamekuwa wakimsapoti na kumueleza kuwa yeye ni mrembo.








Hapo namsifu sana kwani ni shujaa wa ajabu mungu amuongezee subira zaidi na zaidi.
ReplyDelete