Kwa wale waliobwagwa mwaka huu kwa kutoibuka na tuzo hata moja walikuwa na mitazamo tofauti..kuna waliopokea vizuri na wengine hawakufurahishwa na hilo!
Mmoja wa waliopokea tofauti matokeo hayo ni rapa maarufu wa Bendi Totoo Ze Bingwa ambaye alikuwa anawania kipengele cha Rapa bora wa mwaka- Bendi, kipengele ambacho rapa Furgurson kutoka Mashujaa Band aliiibuka mshindi.
Na kupitia ukurasa wa facebook Totoo ameomba asihusishwe tena kwenye tuzo hizo kwa madai ya kudhalilishwa! Soma alichoandika..
''Najaribu kujiuliza ni kwa nini nashirikishwa kili music awards cpati jibu haki ya mungu kwa heshima ya mashabiki wangu naomba kama kutakua na uwezekano nisishirikishwe tena mara 5 ni miaka mitano nimechoka kuzalilishwa''


Totoo .. Chukulia poa tu time itafika, angalia kazi yako.
ReplyDelete