Mwanamke avuliwa nguo hadharani baada ya kushukiwa ni mtekaji,Hii ni sahihi?

Mwanamke mmoja raia wa Nigeria anayeshukiwa kuwa ni mtekaji nyara amefanyiwa kitu mbaya baada ya kuvuliwa nguo zote hadharani na kubaki mtupu huku akipewa kipigo cha haja!

Inasemekana kuwa alikamatwa akiingia kwenye nyumba moja kwa ajili ya kumteka mtoto aliyeachwa peke yake ndani ya nyumba na pia alikutwa na hela ambazo alikiri alizipata baada ya kuuza mtoto mwingine aliyemteka.

Mwanamke huyo anashikiliwa na polisi sasa ila mie swali langu ni sahihi kwa mwanamke kuvuliwa nguo na kudhalilishwa hivi hata kama kakosa? Tena mbele ya watu!

0 Maoni:

Toa Maoni