TANZIA: Pumzika kwa amani Rachel,pigo lingine tena Bongo movie!

Muigizaji wa kike wa filamu za Tanzania (Bongo Movies) anaefahamika kwa jina la Rachel Haule amefariki leo asubuhi (May 27).

Taarifa kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika zinaeleza kuwa muigizaji huyo alikuwa mja mzito na kwamba alijifungua kwa njia ya upasuaji (Operation) jana lakini kwa bahati mbaya mwanae alifariki dunia na yeye hakuwa kwenye hali nzuri.

Imeelezwa kuwa Rachel alipelekwa katika chumba maalumu cha wagonjwa mahututi ( ICU) baada ya hali yake kuwa mbaya sana na leo asubuhi alifariki pia hivyo ni msiba wa mama na mtoto. 


Pumzika kwa Amani Rachel, japo umetangulia njia yetu ni moja! Inalillah wainaillah Rajiun.
Rachel na mchumba wake Saguda ambaye hali yake kwa sasa sijui ikoje maana ikoje maana kupoteza mke na mtoto kwa mpigo sio mchezo!

0 Maoni:

Toa Maoni