Vijana wawili wadogo wamekutwa na mauti baada ya kudondoka kutoka ghorofani walipoandaa party ya kujipongeza baada ya mitihani.
Vijana hao wadogo walianguka mpaka chini walipokuwa kwenye ma-love dove!
Anastasia Tutik,19- raia wa Russia na kijana mdogo mwenye miaka 18 kutoka Mexico aliyefahamika kwa jina moja la Miguel walipoteza balance walipokuwa kwenye balcony baada ya kujaribu kufanya mapenzi.
Wapenzi hao walianguka urefu wa zaidi ya futi 60 kutoka katika floor ya sita na kufariki papo hapo.
Wapenzi hao walikuwa wanajipongeza pamoja na marafiki zao kutoka Bellerbys College,shule ya kimataifa ambayo ada yake inafikia paundi 21,000 kwa mwaka.
Shuhuda wa tukio hilo Samson Oguntayo, 32, amesema vijana hao walikuwa wakijaribu kufanya mapenzi wakati mvulana alipomnyanyua msichana ili kufanya tendo hilo.
Anasema baada ya vijana hao kuanguka alikimbilia eneo la tukio na kukuta wamelala kwenye dimbwi la damu na kuamua kupiga namba ya dharura 999 lakini hata hivyo haikuwezekana kuwaokoa vijana hao.
Miguel alikuwa anachukua kozi ya English akitokea Monterrey na alikuwa anataka kusomea Biashara na Anastasia binti mrembo alikuwa ni mmoja wa wanafunzi bora darasani alikuwa anasoma A level na alikuwa anataka kwenda Chuo Kikuu mwezi September.Alfonso, rafiki wa wawili hao kutoka Mexico,anasema Miguel alifika London wiki moja iliyopita na kukutana kwenye party walipendana na mpenzi wake na kuamua kufanya mambo yao ya mapenzi kwenye balcony.
Baba wa Miguel amesafiri kutokan Mexico na ataingia kesho huko London.





0 Maoni:
Toa Maoni