Baada ya kudaiwa ndio kichuna wa Jay Z nyuma ya Beyonce mwanamuziki Mya afunguka



Zimeibuka taarifa kuwa mwanadada anayefanya muziki wa RnB kitambo Mya ni mpenzi wa Jay Z kwa muda mrefu sasa na amekuwa akimuhudumia kwa kila kitu.

Baada ya kusambaa kwa taarifa hiyo kuna shabiki alimuuliza mwanadada Mya kuhusiana na hilo ambapo kwa hasira alijibu hivi;

"Sijawahi kufanya, sijawahi kuwa na sitakuwa.Huo ni uzushi wa media zenye kiu na habari zisizo na uhakika wala ukweli. Sina mtu wa pembeni..nalipa bili zangu mwenyewe, namiliki management company, namjua Mungu na najiheshimu na kuheshimu ndoa pia siwezi kufanya upuuzi huo''

0 Maoni:

Toa Maoni