Kuna tetesi kuwa Rihanna ambaye kwa muda mrefu kidogo amekuwa single baada ya kuachana na Drake amempata mpenzi mpya, rapper Big Sean.
Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa udaku ‘MediaTakeout’, Rihanna na Big Sean walioenekana Jumamosi (July 5) wakiwa katika pool party a mchezaji wa NBA, Kevin Durant huko Los Angeles.
Mashuhuda walioeleza kuwa na uhakika walidai kuwa wasanii hao walifika katika eneo hilo kwa pamoja na walikaa na kuishi dakika zote kama couple.
Tetesi hizi zinaanza kuaminika na baadhi ya watu kwa kuwa hata Big Sean alishaachana na mpenzi wake Nay Rivera kwa hiyo wote hawana kikwazo cha kuwa wapenzi.


0 Maoni:
Toa Maoni