TANZIA: Msanii wa vichekesho Kenya Jastorina afariki na mama yake afuatia baada ya taarifa za kifo


Mchekeshaji/muigizaji maarufu wa kipindi cha Mashtaka na Jatorina kinachorushwa na Citizen TV, Nancy ‘Jastorina’ Nyambura amefariki Jumamosi (July 26) huku mama yake mzazi nae akifariki baada ya kupokea habari za kifo cha mtoto wake..too sad!

Kwa mujibu wa Citizen TV, Jastorina alikuwa anaumwa muda mrefu ugonjwa wa ‘Meningitis’ na alikuwa akipata matibabu katika hospitali ya Kenyatta nchini humo.

Cha kusikitisha zaidi ni kwamba Jastorina alifariki muda masaa machache baada kutangazwa mshindi katika   tuzo ya Kalasha kama msanii bora wa Ucheshi (Comedy) na ameacha watoto wawili wa kiume.

Mimi pia nilikuwa shabiki mkubwa wa Jastorina hasa alipokuwa akiigiza kama binti wa kazi za ndani wa Mama Kevoo aliyekuwa akimnyanyasa sana kwenye kama series inayoitwa Jastorina,nimepokea kwa majonzi sana jamani...hebu cheki kipaande cha Jastorina hapo chini.

            

0 Maoni:

Toa Maoni