Mwimbaji wa Bongo Flava aliyewahi kuwa mshiriki wa BSS, Meninah amesema anaogopa kuwa katika uhusiano wa mapenzi hivi sasa kwa kuwa anaamini mapenzi yatavuruga muziki wake.
Akiongea na mie katika kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm, Meninah ameeleza kuwa hivi sasa yuko single na hajawa na mpango wa kuingia katika uhusiano kutokana na sababu hizo.
Kwa sasa niko Single naangalia kazi yangu kwanza... Nikiingia kwenye mahusiano kazi yangu itakuwa shaghala bagala.” Amesema Meninah.
Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa mwimbaji huyo ana ukaribu na Diamond lakini alikanusha na kueleza kuwa hajawahi hata kuwa na ukaribu na mkali huyo.
Unaweza kuwa umeshasikia na unaamini Meninah yuko kwenye uhusiano na….. Lakini msikilize pia yeye. “Unajua watu wanaamini ukiwa msichana mzuri basi ni lazima uwe katika uhusiano!”
Meninah ameachia wimbo mpya unaoitwa ‘Pipi ya Kijiti’.
![]() |
| Mie na Meninah studio alipokuja kwa ajili ya interview leo |
![]() |
| Meaninah na Dj Rguy |



0 Maoni:
Toa Maoni