Nimekutana na habari hii ya kusikitisha nikaamua ku-share nawe msomaji wa MamuAfrica blog, stori ya vijana wawili waliopendana ila tu kutokana na kushindwa kuwa pamoja huku sababu ya tofauti za kimila ikitajwa wakaamua kuyakatisha maisha yao kwa pamoja.
Charleigh Disbrey (15)au alifahamika sana kwa marafiki zake kama kama CJ alifariki na boyfriend wake Mturuki mwenye miaka 18-Mert Karaoglan huko Borehamwood, Hertfordshire.
Kwa mujibu wa UK Mirror, wapenzi hao wadogo walipanda juu ya fensi na kujirusha kwenye treni lakini muda mfupi kabla ya kujiua Mert aliwatumia marafiki zao picha inayowaonyesha wawili hao wakitabasamu huku wamesimama kwenye daraja kando ya reli.
Pia aliwatumia ujumbe marafiki kuwaambia waitafute simu yake ambayo ilieleza 'Hatuwezi kuwa pamoja katika maisha haya na bora tuwe pamoja katika sehemu tofauti' !

0 Maoni:
Toa Maoni