Mchezo wa maisha halisi ndani ya jengo moja la Big Brother Africa unaendelea huku washiriki kadhaa wakiondolewa mjengoni ikiwa ni safari ya kumpata mshindi wa msimu huu uliopewa jina la ‘Hot Shots’
Jana jumapili mshiriki wa Tanzania Irene Laveda aliukwepa moto na kuwashuhudia Esther (Uganda), Sabina (Kenya) na Lilian (Nigeria) wakiondolewa katika mchezo huo...washiriki ambao sikuwafikiria kama watatoka aisee!
Hadi sasa ni washiriki wa kike 8 na wa kiume 13 waliobaki katika jengo hilo huku Tanzania ikiendelea kuwakilishwa na washiriki wote wawili.
Nchi za Uganda, Zambia, Msumbiji, Kenya na Nigeria hivi sasa zinawakilishwa na mshiriki mmoja mmoja baada ya washiriki wengine kuondolewa.

Huu mchezo wanao tazama watoto wa masaki
ReplyDelete